Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Kongamano lenye kubeba anuani hii: “AhlulBayt (a.s), Haki na Heshima ya Kibinadamu” limefanyika katika mji wa Abidjan, nchini Ivory Coast, likihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s), Ayatollah Reza Ramezani.
Kongamano au Mkutano huu uliandaliwa na tawi la Jāmi‘at al-Mustafa International University nchini humo, kwa lengo la kueneza mafundisho ya AhlulBayt (a.s) na kukuza thamani za kijamii kama uadilifu na heshima ya kibinadamu.
Ayatollah Ramadhani amefika Ivory Coast kwa mwaliko wa viongozi wa kidini wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kimataifa yenye malengo ya kuimarisha uhusiano wa kitamaduni na kielimu na jamii za Waislamu barani Afrika.
Your Comment